Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, katika hali ya kupanda kwa bei za nishati na kupungua kwa ukuaji wa uchumi, serikali za Umoja wa Ulaya zinajiandaa kwenye mgogoro ambao ni vigumu kuudhibiti; mgogoro ambao unaweza hata kudhuru “mkondo mkuu wa kisiasa” katika nchi hizi. Seamus Boland, rais wa Kamati ya Kiuchumi na Kijamii ya Ulaya, alisema: Gharama za kuongezeka kwa nishati zinaenea hadi kwenye chakula, usafiri na makazi. Siku hizi amekuwa akikusanya vyama vya wafanyakazi kutoka kote Ulaya na kutoa ushauri kwa Tume ya Ulaya kuhusu sera za kiuchumi na ajira.
Kwa mujibu wa kauli za Valdis Dombrovskis, kamishna wa uchumi wa Ulaya, athari za mzingiro wa lango la Hormuz zinazidi kuonekana wazi na “zinaenea katika uchumi wa dunia.” Ustahimilivu wa kifedha na kiuchumi umekuwa ukijaribiwa mara kadhaa tangu mgogoro wa COVID-19 na pia tangu mgogoro wa kwanza wa nishati, lakini safari hii ni ngumu zaidi kuliko wakati wowote uliopita.
Hapo awali, Dombrovskis alikuwa ameonya kwamba, nchi za Umoja wa Ulaya zinaweza kukumbwa na mdororo wa uchumi, yaani mfumuko mkubwa wa bei sambamba na ukuaji mdogo wa pato la taifa na kuongezeka kwa ukosefu wa ajira barani Ulaya.
Makadirio ya hivi karibuni yanaonyesha kuwa, iwapo bei za nishati zitarejea katika viwango vya kabla ya vita hadi mwisho wa mwaka 2026 (jambo ambalo linaonekana kuwa lisilowezekana), ukuaji wa pato la taifa (GDP) utakuwa kwa kiwango cha juu asilimia 0.4 chini ya utabiri wa sasa. Ikiwa bei za mafuta na gesi zitaendelea kuwa juu, hali hiyo itakuwa mbaya zaidi. Katika hali ya kwanza, mfumuko wa bei unatarajiwa kufikia 3%, na katika hali ya pili unaweza kufikia 4.5%.
Chanzo: TASS
Maoni yako